Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga amesema pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika kusema Yanga haijapewa wachezaji na Singida United, wao wanasisitiza wamewapa wawili.
Sanga amesema ameshangazwa na kauli ya Nyika kuwa ni mtu aliyesema maneno yasiyo sahihi.
“Yanga wamepewa Deus Kaseke na Fei Toto na awali walilisema hili. Lakini inashangaza sana kuona anasema kuwa hawajapewa.
“Sielewi alikuwa ana maanisha nini, au anataka kusema Yanga imetumia fedha kuwapata, sidhani. Kama kuna jambo awaeleze wanachama wake lakini Mheshimiwa Mwigulu amewapa Yanga hao wachezaji,” alisema Sanga.
Siku mbili zilizopita, Nyika alieleza kuwa Yanga haipewi wachezaji kama ambavyo imekuwa ikielezwa na badala yake inafanya usajili kufuata matakwa ya mwalimu kwa kutumia fedha zake.
KLABU YA YANGA INAHUJUMIWA YAANI KUNA "KIRUSI" PALE YANGA SIJUI NI NANI INAWEZEKANA MTANDAO HUU UMESUKWA KWA MUDA MREFU...UNAMUHUSISHA KOCHA MWINYI ZAHERA, HIVI HUYU KOCHA ATAWEZAJE KUKATAA BEKI AMBAYE ANAKUJA KUZIBA MAPENGO YA NAMBA 2 NA TANO? UNAACHA WACHEZAJI, HALAFU UNAPEWA BEKI MZIMBABWE BURE HALAFU UNAMKATAA...KWELI? HAYA UNAWAACHA WACHEZAJI AMBAO WAMEKUHUDUMIA MSIMU MZIMA KWA KUTOLIPWA MSHAHARA.....BADO HAUJAFANYA USAJILI WA KUZIBA MAPENGO YA WACHEZAJI WALIONDOKA...BEKI NAMBA 2 NA 5, WASHAMBULIAJI NAMBA 9, 10, 11, KIUNGO NAMBA 6....HALAFU UNATAKA WATANZANIA ASILIMIA 55% AMBAO NI WAPENZI WA KLABU WAJE UWANJANI, KUANGALIA TIMU IPI? NATABIRI MAPATO YA UWANJANI KUPOROMOKA, HAMASA YA KWENDA KWENYE MECHI KUPUNGUA....HATIMA YA SOKA LA TANZANIA KUPOROMOKA..
ReplyDeleteAchana na nyika analeta siasa kwenye ukweli km wana hela wasingeshinda kumpa kesi milioni mbili na baskeli ili wamsajili
ReplyDeleteFei hajawahi kua mchezaj WA singida. Kaseke alimaliza mkataba. Wamewapaje yanga wachezaji? Klab gan duniani inaweza inawapa wapinzani wake wachezaji.
ReplyDelete