July 17, 2018


Kikosi cha Yanga kimewasili salama jijini Nairobi Kenya kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC.

Kikosi hicho kimewasili Nairobi bila ya wachezaji Hassan Kessy na Kelvin Yondani ambao imeelezwa wamegoma wakishinikiza kuongezewa mikataba.

Yanga watacheza na Gor Mahia Jumatano ya Julai 18 2018 wakiwa na kibarua kikali cha kuhakikisha wanapata alama tatu ili kujiwekea nafasi ya kusonga mbele kuelekea hatua nyingine.

Katika kundi D ambalo Yanga wapo na MC Alger, Rayon Sports na Gor Mahia ambao watacheza nao kesho, wana alama moja pekee waliyoipata dhidi ya Rayon Sports iliyopigwa Uwanja wa Taifa kwa matokeo ya sare ya 0-0.

Mechi hiyo itachezwa majira ya saa 10 kamili jioni kwa mujibu wa ratiba ya CAF kwenye Uwanja wa Machakos jijini Nairobi.

2 COMMENTS:

  1. HIVI YANGA MBONA MNATUAIBISHA HIVI.....MIMI NITAANDIKA BARUA TFF ILI ITOE ONYO AMA KUWAADHIBISHA VIONGOZI WA TIMU ZOTE ZINAZOSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA, KAMA HAKUNA MAANDALIZI YA KUTOSHA , NA KUWA KAMA WACHEZAJI HAWAPEWI MAANDALIZI MAZURI, MAZOEZINI, MALIPO NA MOTISHA NZURI, SAFARINI KUKOSA WACHEZAJI MUHIMU, MWISHONI KATIKA MECHI AMBAPO WANAWAKILISHA NCHI NA KUBEBA BENDERA YA NCHI.....MWISHONI KUISHIA KUFUNGWA AIBU SIO KWA YANGA TU BALI TAIFA ZIMA...RAISI MAGUFULI NAKUMBUKA ALISEMA IFIKE MWISHO TIMU ZETU ZISIWE ZINAISHIA KUFUNGWA FUNGWA TU, NI AIBU SANA...IFIKE MWISHO SASA. YANGA HAWAKUSHIRIKI CECAFA WAKISEMA WACHEZAJI WAO HAWANA MIKATABA, NA WAMEPEWA RUHUSA YA KUPUMZIKA, SASA CAF IMEFIKA NAPO BADO KUMBE HATA MIKATABA HAWAJAPEWA NA WENGINE WANAGOMA, MAJINA YA WACHEZAJI WATATU YAMECHELEWA CAF, HAYA BADO USAJILI UNASUASUA HUU NI UPUUZI MKUBWA....HAIVUMILIKI LAZIMA VIONGOZI WOTE WAJIUZULU.....TUNAKWENDA KUIAIBISHA NCHI...KUNA HAJA GANI YA YANGA KUSHIRIKI MASHINDANO HAYA IKIWA KWAMBA WANAENDA KUPELEKA KIKOSI KISICHO IMARA...WATANZANIA IMEFIKA WAKATI TUSIWE TUNATEGEMEA MIUJIZA, AU BAHATI...MPIRA NI SAYANSI NA MAANDALIZI, NA MOTISHA KWA WACHEZAJI NA BENCHI LA UFUNDI.....USANII NA USWAHILI SWAHILI UFIKE MWISHO....WAPENZI WA SOKA TANZANIA TUMECHOKA KUWA WASINDIKIZAJI NA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU JAMANI......

    ReplyDelete
  2. JUMATANO KESHO TIMU INACHEZA KULE KENYA ACHENI KULETA MANENO YA KUWAKATISHA TAMAA WACHEZAJI NA VIONGOZI WA TIMU YETU WOTE INAYOWAKILISHA NCHI MUHIMU KUWATIA MOYO NA KUWAOMBEA WAFANYE VIZURI

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic