July 28, 2018


Kutokana na hali ya Yanga kuwa katika kipindi cha mpito hivi sasa, imeelezwa kuwa Katibu wa Baraza la Wazee ndani ya klabu hiyo, Ibrahim Akilimali, amepanga kufika Ikulu kwa Rais John Pombe Magufuli.

Taarifa imeeleza kuwa Akilimali amefunguka na kusema njia pekee ya Yanga kuepukana na hali iliyonayo kwa sasa ni kupata msaada wa Rais Magufuli ili kuikomboa iweze kurejea kama ilivyokuwa zamani.

Akilimali ameeleza kuwa Yanga haijaanza leo kuwa na migogoro bali tangu kipindi cha utawala wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hivyo si kitu kigeni kinachotokea hivi sasa.

Aidha, Katibu huyo amesema alikuwa mtu pekee aliyepinga klabu hiyo kukodishwa na akieleza chanzo cha migogoro ndani ya timu hiyo kuanza kushika kasi kilianza kipindi hicho.

Mzee huyo amesema kwa sasa anafanya namna ya kuweza kukutana na Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete ili aweze kumfanyia mpango wa kukutana na Magufuli ambaye anaamini anaweza akawa msaada mkubwa kuisaidia Yanga.




3 COMMENTS:

  1. Ameibukia!!!! Kumbe hata mpango bado haujakamilika. Toa hii sehemu ya comments kama huwa hufuatilii hadhira yako inataka vitu gani. Huna habari zingine za kuandika si unakaa kimya tu lakini sio kuandika nonsenses.

    ReplyDelete
  2. Kwani di ndoo yeye aliyepinga Manji kukodishwa yanga na akasema yanga itajiendesha bila ya Manji na ilifika wakati wakimtaka Manji akae upande waiendeshe wenyewe timu na ni hvi karibuni alitamka kuutaka yeye uraisi akiahidi kulipa mishahara ya wachezaji kwa wakati kwakuwa pesa ziko na imekuwaaje sasa kumtska Rais Magufuli aingilie je anakusudia kuingilia kwa kulipa mishahara ya wachezaji au afanikishe kuwekwa yeye badala ya Manji na bado akitamka kuwa ni yeye aliyepinga yanga kukodishwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic