July 28, 2018


Baada ya kikosi cha Yanga kitakachotumika katika msimu wa 2018/19 kuwekwa hadharani huku jina la kipa Mcameroon, Youthe Rostand kuwa katika orodha, gumzo kubwa limeibuka kwa mashabiki wa klabu hiyo dhidi ya kipa huyo.

Rostand amejumuishwa katika wachezaji ambao watakuwepo Yanga msimu ujao huku uwepo wake ukiwaibua mashabiki wengi wa Yanga wakiutaka uongozi waachane naye.

Awali kulikuwa kunaelezwa Rostand angeweza kupelekwa kwa mkopo mahala pengine lakini kitendo cha kutajwa kuwa sehemu ya kikosi hicho katika msimu ujao kimewashangaza mashabiki wengi wa Yanga.

Mashabiki hao baadhi wamesema kiwango cha kipa huyo kimeshuka hivyo wamezidi kuomba vema akaondoshwa au apelekwe kwa mkopo mahala pengine ili kuweza kuimarisha vema uwezo wake langoni.

Kipa huyo aliyesajiliwa kutoka African Lyon ilielezwa angeweza kurejeshwa katika timu hiyo kwa mkopo japo ikaelezwa aligoma akidai ni vema Yanga wakavunja mkataba wake kisha wampe chake ili aweze kuondoka.

Baada ya Rostand kugoma, inaonekana kama Yanga wamegoma kuvunja mkataba wake kwa hofu ya kula hasara hivyo amejumuishwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wataendelea kuwepo na timu hiyo msimu ujao.

1 COMMENTS:

  1. Jamani kusoma hamjui hata picha hamuoni.yanga haina pesa iweje imlipe rostand aliegoma kupelekwa kwamkopo.maana yake ili umuache nikuvunja mkataba jambalo litapelekea club kulipa pesa nyingi nibora kuvumilia maumivu kuliko kukosa hata kupeleka timu kumalizia mechi ya gor

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic