July 13, 2018


FulTime: Dakika 90 zimemalizika, Azam wanafanikiwa kuutetea ubingwa wao kwa mara ya pili mfululizo.

Dak ya 90, Zimeongezwa dakika 4 mpira kumalizika
Dak ya 89, Kipa Razak anaenda kupiga, piga kule, mpira unakwenda nje
Dak ya 87, Penatii, Azam wanapata penati baada ya mshambuliaji wao kufanyiwa madhambi eneo la hatari
Dak ya 85, Mohamed Rashid anapiga shuti kubwaa linapaa juu ya lango la Azam FC
Dak ya 85, Faulo inapigwa kuelekezwa Azam FC, dakika 5 zimesalia mpira kumalizika

Dak ya 84, Ndemla anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Moses Kitandu
Dak ya 80, Chilunda anaumia, anabebwa na Machela kupelekwa nje ya Uwanja
Dak ya 78, Dakika zinazidi kwenda, bado Azam wanaongoza kwa mabao 2-1
Dak ya 77, Rashid Juma anakosa kumalizia krosi safi kwa kichwa na badala yake inakwenda nje
Dak ya 75, Simba wanaanza upya kwa mpira wa kurushwa baada ya Azam kuutoa, Wawa anampasia Juma, naye anaupeleka kwa Bukaba
Dak ya 73, Ndemla anapewa kadi ya njano baada ya kucheza madhambi

Dak ya 71, Mzamiru Yassin ametoka nje kugangwa baada ya kuumia, dakika zinayoyoma
Dak ya 68, Piga kule Morris, goooooli, Dida unamshinda mpira na sasa Azam wannakuwa mbele kwa mabao 2-1
Dak ya 67, Azam wanapata faulo kuelekea Simba,
Dak ya 67, Kagere tena na mpira kuelekea langoni mwa Azam, piga krosi moja kipa Eazak anadaka mpira na kulala

Dak ya 62, Simba wanaanza kwa kasi kati mwa Uwanja, piga kwake Kageree, Goooooooli, anasawazisha, sasa ni 1-1
Dak ya 61, Mpira sasa upo katikati ya uwanja, Azam wanatafuta mbinu ya kuipenya ngome ya Simba kuongeza bao la pili
Dak ya 59, Rashid Juma anaingia kuchukua nafasi ya Marcel Kaheza
Dak ya 59, Kahezaaa, piga kanzu moja kwa kipa wa Azam lakini inatua juu ya nyavu
Dak ya 57, Azam wameanza kuja juu tena katika lango la Simba, Chilunda anapiga mashine inagonga mwamba

Dak ya 56, Faulo inapigwa kuelekea Azam
Dak ya 54, Bukaba anatoka nje kutibiwa baada ya kuumia
Dak ya 33, Offside, Kaheza anaotea, Simba wanazidi kupambana kusaka bao la kusawazisha
Dak ya 52, Tayari mpira umeshaanza, pigwa krosi moja huku katika lango la Azam, Kaheeza, anapiga nje
Dak ya 51, Kangwa anaonekana kuchechemea huku akitolewa nje kugangwa, mpira umesimama kwa muda

Dak ya 50, Simba wanapata nafasi ya kutengeneza bao lakini kunakuwa hakuna mawasiliano mazuri mbele baada ya Kaheza kutengeneza nafasi nzuri
Dak ya 48, Bukaba anatoa mpira nje, unarushwa kuelekezwa Simba
Dak ya 47, Wawa anapiga mbele kumtafuta Mohammed Hussein lakini anachezewa madhambi na mpira unakuwa faulo, pigwa kule lakini inakwenda nje
Dak ya 46, Kaheza anamchezea rafu Singano, faulo inapigwa kuelekea Azam FC
Dak ya 45, Dakika 45 za awamu ya pili zinaanza Uwanja wa Taifa

HALF TIME: AZAM FC 1-0 SIMBA SC

Dak ya 45, Imeongezwa moja kuelekea mapumziko
Dak ya 43, Mpaka sasa simba wamecheza faulo 9 na Azam wakicheza 12
Dak ya 42, Simba wanarusha mpira kuelekea Azam, kwake Kagere, unakuwa wa kurushwa kuelekezwa Azam
Dak ya 40, Simba wanahaha kusaka bao la kusawazisha lakini beki ya ulinzi Azam imekuwa imara
Dak ya 37, Simba wanapata faulo, anapiga Kaheza, piga shuti lakini mabeki Azam wanaokoa na kutoa mpira nje, inakuwa kona, anaenda Kaheza kupiga lakini inatokea faulo, mpira unapigwa kuelekea Simba

Dak ya 36, Singano tena, kwake Domayo, anaupeleka kwa Wadada, naye anampasia Nchimbi, Azam wanang'ara sasa
Dak ya 35, Mpira anaoa Razak akiwaambia wachezaji wake waende mbele, mpira unapigwa kwake Wadada, unakwenda kwake kule Domayo
Dak ya 32, Kona tena, awamu hii inapigwa kuelekezwa Simba, ni ya tatu, pigwa huku na Singano, gooooooli, Chilunda anaifungia Azam bao la kwanza
Dak ya 31, Mashabiki wa Simba wanashangilia kwa nguvu kuipa mroali timu yao

Dak ya 20, Kaheza anapiga, piga moja juu Razak anaruka kama nyani anaokoa na kulala chini baada ya kubabatizana na Bukaba
Dak ya 28, Gyan anaanza upya kwake Bukaba, piga mbele huku inakuwa kona, ni ya kwanza kwa Simba
Dak ya 26, Wawa sasa na mpira, piga mbele huku kwenda kwake Ndemla lakini unakataa
Dak ya 24, Mpira unarushwa kuelekea Azam, Gyan amerusha, kwake Kagere, anapiga krosi lakini unakwenda nje

Dak ya 23, Hatari katika lango la Azam, mabeki wanakuwa imara wanaokoa mpira
Dak ya 23, Tayari imeshapigw lakini inakosa madhara, Dida anaokoa
Dak ya 22, Kona wanapata Azam ni ya pili huku Simba wakiwa hawajapata hata moja
Dak ya 22, Mohammed Hussein anarusha mpira kuelekea lango la Azam, bado milango ni migumu.

7 COMMENTS:

  1. Poleni Simba, pole Hajira Manara

    ReplyDelete
  2. simba tunatia aibu sana sijui kwann tunafungwa hovyo??????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nina shaka nawe , ungekuwa simba usingesema hayo ,simba ipi inayofungwa ovyo?wangefungwa hovyo wasingefika fainali ,sio kulaumu kila mara .

      Delete
  3. kikosi imara tatizo liko wapi?mbona kila siku majanga?

    ReplyDelete
  4. Dida ataikosti sana Simba, Wawa na Bukaba hawaelewani kwenye kona na kucheza krosi, beki namba tatu uchochoro hayo ndiyo mapungufu niliyo yaona

    ReplyDelete
  5. Duuuuh! Simba vipi jaama,nausajili wote huo wa mamilion bado mnadedeeeeema, mtasingizia wachezaji hawakuepo):

    ReplyDelete
  6. Simba gani lakini mnayoizungumzia? Nashindwa kufahamu. Ni ile simba halisi ya akina john Boko,Manula, Okwi, kapombe, kwasi au hii simba ya majaribio iliocheza fainali za kagame?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic