July 6, 2018


Wakati klabu kongwe ya Yanga ikikumbwa na sakata la uhaba wa fedha hivi sasa, Ofisa Habari wa Simba ameyataka matawi yote ya Simba kuichangia Yanga.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika akiwataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuanza kuichangia Yanga kwa maana hali ya kiuchumi hivi sasa si rafiki.

Msemaji huyo mwenye maneno mengi amesema Yanga imejitakia kufikia hali iliyonayo hivi sasa mpaka akafikia hatua ya kutoa agizo kwa Wanasimba kutoa mchango wao uweze kuwasaidia.

Sisi si maadui wala mahasimu, sisi ni watani tena wa jadi, kwa maana hiyo na kwa kutumia mamlaka niliyopewa naagiza matawi yote ya Lunyasi nchi nzima wachange kunusuru ufakiri huu wa kujitakia walionao jamaa zetu. Hili ni agizo si hiari, na mimi ninaanza kwa kutoa milioni tano leo" mameandika Manara.


7 COMMENTS:

  1. Yapo mambo ya maana ya kuzungumzia Simba mfano ujenzi wa uwanja n.k achana na utani huo hauna tija,

    ReplyDelete
  2. Manara punguza utani wana yanga watakulilia ukiacha kutoa hiyo milion tano wanategemea ukitoa hiyo ml tano watasajili hata wachezaji watano wa milion mojamoja

    ReplyDelete
  3. Manara ukweli yanga wanahali ngumu sana,usiwatamanishe watakuja kuzifuata hizo m.tano.

    ReplyDelete
  4. Wachange wajenge uwanja c kuichangia Yanga,kweli maskini akipata .......hulia mbwata

    ReplyDelete
  5. Manara alichangiwa na wanayanga alipougua baada ya kukosa Msaada kwa wanasimba wenzake. Baada ya kupona Leo umekuwa jeur sana.

    ReplyDelete
  6. MANARA YUPO FIELD BAADA YA MATIBABU MIREMBE KWAHIYO MSISTUKE SANA, KAMA HALI YAKE BADO INATATANISHA BASI MADAKTARI WATAJUA WAPI PA KUENDELEA NA MATIBABU. MUOMBEENI TU APOTE HAYO MATATIZO YAKE YA AKILI

    ReplyDelete
  7. Manara is never worrieed. He is always happy and smiling. Smile with world because smiling symbolizes friendship, love and peace

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic