Baada ya kumalizana na Simba, mshambuliaji Laudit Mavugo anaweza kupata nafasi ya kukipiga katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Mavugo raia wa Burundi, tayari kupitia meneja wake, ameanza mazungumzo na Baroka FC anayoichezea Mtanzania, Abdi Banda.
Mmoja wa maofisa wa Baroka FC, amesema wanaendelea na mazungumzo na Mavugo.
“Ni kati ya klabu na uongozi wa Mavugo, kwa sasa siwezi kusema jambo hadi tutakapofikia hatua nzuri,” alisema.
Mavugo akiwa Simba, alishindwa kuonyesha cheche zake hasa katika upachikaji mabao na mara kadhaa alionyesha matumaini lakini akashindwa kuendelea.
Kwa sasa Banda ndiye tegemeo la Baroka FC katika ulinzi na kama Mavugo ataungana naye, itakuwa wanacheza pamoja kwa mara ya pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment