July 5, 2018


Baada ya wachezaji 8 kutupiwa virago juzi na Mkongomani wa Yanga, Mwinyi Zahera, Kocha huyo ameamua kuwapitisha watano akiwemo Mrisho Ngassa, imeelezwa.

Ngassa aliyetua Jangwani akitokea Ndanda FC, amemridhisha Zahera kutokana na namna anavyojituma Uwanjani kitu ambacho kimepelekea kumshawishi Mkongo huyo kumpitisha.

Mbali na Ngassa, straika aliyetua hivi karibuni na kuviteka vyombo vya habari nchini, Mnigeria, Emeka Emaruni, amekuwa miongoni mwa miongoni mwa waliomridhisha Kocha Zahera ikielezwa amewaambia mabosi wake wampe mkataba.

Aidha, Zahera amefurahishwa na kiwango cha Heritier Makambo aliyewasili nchini siku chache zilizopita kwa siri kubwa akitokea DC Motema Pembe ya DR Congo.

Achana na Makambo, Mkongo huyo imeelezwa pia ameshajuza viongozi wa juu wa Yanga juu ya kiungo Jaffary Mohammed aliyetokea Majimaji FC baada ya timu hiyo kushuka daraja msimu uliopita.

Mchujo huo umekuwa ukifanyika ili kupata wachezaji ambao wataweza kuisaidia Yanga kwa ajili ya mashindano ya kimataifa na Ligi Kuu Bara ambapo kikosi kimekuwa kikijifua kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini, Dar es Salaam.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic