July 22, 2018


KMC FC imedhamiria kukiboresha kikosi chake kulekekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara ambapo winga aliyekuwa akiichezea Mbao, James Msuva, amekamilisha usajili kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo.

James ambaye ni mdogo wake na Simon Msuva, amemalizana kila kitu na mabosi wa KMC ambapo sasa ataonekana na uzi wa klabu hiyo mpya iliyopanda daraja kushiriki Ligi Kuu msimu unaoanza mwezi Agosti 2018.

Msuva ameungana na Mrundi Yusuph Ndikumana ambaye pia aliwahi kuichezea Mbao baada ya kusaini na KMC miezi kadhaa iliyopita akiungana na Kocha Etienne Ndayiragije kutoka Burundi pia.

Ndayiragije sasa ameuamua kukibomoa kikosi cha Mbao baada ya kumnasa Msuva ambaye ametajwa kuwa ni pendekezo lake ili kukipa makali kikosi chake hicho dhidi ya wapinzani pale msimu mpya utakapoanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic