July 10, 2018


Nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo yupo mbioni kusaini mkataba wa miaka minne muda mchache kuanzia hivi sasa na klabu ya Juventus ya Italia kwa dau la dunia.

Dau kubwa la fedha lenye thamani pauni milioni 105 ndiyo limetajwa kumuondoa Ronaldo Real Madrid baada ya kuichezea kwa mafanikio makubwa tangu ajiunge nayo akitokea Manchester United.

Kuondoka kwa Ronaldo kumekuja mara baada ya makubaliano ya viongozi wa pande zote mbili pamoja na mchezaji ambaye mwenye aliomba kuondoka ili kubadilisha mazingira na pengine kumalizia maisha yake ya soka nchini Italy.

Uhamisho huo wa Ronaldo kwenda Juventus utakuwa unaweka rekodi ya dau kubwa kuwahi la usajili kutokea duniani likizidi lile la Neymar kusaini PSG kwa euro milioni 222.

Kushindwa kufikia makubaliano na Rais wa Madrid Fiorentino Perez, ya kuongeza mkataba na Ronaldo yamechagiza mchezaji huyo kuondoka kutokana na dau kubwa alilokuwa akilihitaji.

Aidha, ilielezwa pia tetesi za ujio wa Neymar Real Madrid kuwa ni sababu mojawapo za nyota huyo kutaka aondoke kuelekea mahala pengine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV