July 11, 2018


Shirikisho la Soka Tan­zania (TFF), limepanga kuongeza idadi ya wachezaji wa kimataifa kwa klabu za Ligi Kuu Bara kutoka saba na kufi­kia kumi katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Hiyo itakuwa nafasi pekee kwa klabu kongwe za Simba na Yanga ambazo zimekuwa zikilalamikia kubanwa usajili wa profesheno wachache hapo awali.

Simba tayari hadi hivi sasa ina wachezaji nane wa kimataifa ambao ni James Kotei, Emmanuel Okwi, Asante Kwasi, Nicholas Gyan, Haruna Niyonzima, wengine wal­iowasajiliwa hivi karibuni ni Pascal Wawa, Meddie Kagere na Fabrice Kakule.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, shirikisho hilo limepanga kuanza kutumia kanuni hizo katika msimu ujao wa ligi ili kuhakikisha wawak­ilishi wa michuano ya kimataifa wanakuwa na kikosi cha wachezaji wengi profesheno wenye uzoefu.

Mtoa taarifa huyo alisema, wakati shirikisho hilo likitangaza kuongeza idadi hiyo ya wachezaji tayari limetoa sharti la kutumia nyota saba pekee katika kila mchezo wa ligi huku mashindano ya kimataifa likiwaruhusu kutumia wowote watakaohitaji.

“TFF limepanga kuongeza idadi ya wachezaji wa kimataifa kutoka wachezaji saba hadi kumi katika kuelekea msimu ujao wa ligi.

“Tayari klabu zimeanza kupewa taarifa za usajili huo wa wache­zaji wa kimataifa, lengo kubwa ni baadhi za klabu kuziimarisha timu zao katika kuelekea michuano ya kimataifa.

“Kanuni hizo za wachezaji kumi ziliwahi kutumika misimu mitano iliyopita ya ligi kwa TFF kutoa na­fasi ya kusajili idadi hiyo ya wache­zaji ambayo tunaamini siyo ngeni,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, kuzungumzia hilo simu yake ya mkononi iliita bila ya mafanikio ya kupokelewa, lakini Championi linafahamu tayari viongozi wa klabu wameshapewa taarifa.

CHANZO: CHAMPIONI

4 COMMENTS:

  1. Mmh!!!hili ndio soka la bongo team flan ikiwa na watu wake madarakan watafanya kutokana na matakwa ya team yake kipenz ......

    ReplyDelete
  2. 😂😂😂😂 ungekuwa muwazi tu kuandika TFF waibeba simba

    ReplyDelete
  3. Ni zuri lkn litakaa kwa kipindi kifupi kwa kuwa sio hitaji la mpira wetu kwa ujumla.
    Ni hitaji la timu Fulani kwa kipindi Fulani.

    ReplyDelete
  4. Kama kweli TTF wana nia ya kweli ya kuifanya ligi yetu kuwa na ushindani wa kweli na kunyanyua viwango vya wachezaji wetu wa ndani basi hakuna haja ya kuvizuia au kuviekea masharti vilabu vyetu idadi ya wachezaji wakigeni wa kuwachezesha uwanjani kwa wakati mmoja. Mimi naona TTF kama imemua kujitwanga risasi ya mguu wenyewe kwani lengo hapa ni kuwa na ligi yenye ushindani itakayozalisha wachezaji watakaokuwa na uwezo wa kupambana kimataifa watakaoibeba Taifa Stars. Binafsi naona idadi ya wachezaji wakigeni iongezwe wawe 12 na timu iruhusiwe kuchezesha idadi yeyote ile ya wageni uwanjani na kama watatokea wazawa wa kuwachomesha mahindi wachezaji wa Taifa wa kenya, uganda au hata Rwanda basi utakuwa mwanzo mzuri wa kuwa na taifa stars ya ushindani. Hakuna haja ya kuwajengea mazingira ya uoga wachezaji wetu katika kushindana kwani tumeshafanya hilo zoezi la idadi ya wachezaji na hali inazidi kuwa mbaya kwanini tusije na mkakati mbadala?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic