July 11, 2018


Uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka kuhusiana na usajili wa kiungo mshambuliaji, Issa Mohammed Banka aliyetia kandarasi ya miaka miwili na mabingwa hao wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara.

Kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Hussein Nyika, amesema kuwa mchezaji huyo waliyemsajili kutokea Mtibwa Sugar amekuwa na mchango mkubwa ndani ya Uwanja.

Nyika ameeeleza kuwa hakuna asiyejua mchango wa Banka kutokana na umahili wake wa kutandaza soka kuwalisha mipira washambuliaji wa mwisho, kitu ambacho kimepelekea wao kumsajili.

Aidha, Nyika anaimani Banka atakuwa msaada ndani ya kikosi cha Yanga ambacho kinajiandaa hivi sasa kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya.

Kuelekea mechi hiyo kubwa ya mkondo wa kwanza, Yanga itasafiri kwenda kuanzia Kenya ambapo itacheza dhidi ya mabingwa hao watetezi jijini Nairobi Julai 18 2018.

2 COMMENTS:

  1. Usajili wa ndani unaisha tarehe 20 July. Sasa hata wachezaji wa kigeni mpaka sasa zimebaki siku 10 hawajasajiliwa mnawadanganya watu kuwa eti mpaka mwalimu awajaribu huo ni uongo mnajenga hoja kwamba kocha mpaka ampitishe mchezaji wa kigeni ila ukweli ni kuwa wachezaji wengi hawasajili Yanga kwani mnataka kuwapiga 10%. Kuna hatari mkashindwa kupata mchezaji wa kigeni kwani muda unaisha. CAF wametoa mpaka August 4, lakini ni kufanya uhamisho wa mchezaji wa kigeni. Kuna hatihati Mnigeria akawa kama mbenini, kiungo na beki mkongo anayesemekana anakuja Yanga, anayeitwa Yannick Litombo amefikia wapi? Naye pia anafanya majaribio au? Na ataanza lini ikiwa mwisho wa usajili ni August 4, na Julai 20?

    ReplyDelete
  2. Ama kweli Uongozi wa Yanga Unachekesha,Kipindi chote ambacho wanasema wanasajili kimya kimya usajili wenyewe ni hao wanne tu kipindi chote hicho,waache utani watafute fedha wasajili wachezaji sio utaniutani huo,muda hauwasubiri

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV