WANACHAMA YANGA NAO WAIBUKA JUU YA SAKATA LA TARIMBA NA KLABU YAO, WAMEELEZA HAYA
Baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga wameibuka na kueleza sakata la aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum kuivusha Yanga wakati wa mpito, Abbas Tarimba kujizulu kwake.
Wanachama hao wameeleza suala hilo wakisema Tarimba hakupaswa kuondoka moja kwa moja Yanga na badala yake alipaswa kuzungumza na viongozi wenzake ambao yupo nao pamoja.
Mwanachama mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema kitendo alichofanya Tarimba kimempa uwalakini kutokana na kujiondoa kwake, huku akishauri kuwa alipaswa kukaa na wenzake ili wayamalize.
Wakati hao wakishangazwa na Tarimba kujiondoa, wengine pia wamefunguka na kusema uongozi wa Yanga umekuwa hauna watu wa mpira kitu ambacho kimesababisha Tarimba kujiondoa.
Tarimba mabaye aliteuliwa kupitia Mkutano Mkuu wa Yanga Juni 10 2018, juzi alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na kutokuwa na maelewano na baadhi ya viongozi wa Yanga katika kutekeleza majukumu ya Kamati aliyopewa.
Tarimba alieleza kuwa viongozi wa Yanga ni waongo hivyo ni vema wakamuacha aendelee na mambo yake mengine kutokana na namna mwenendo wa sehemu hizo mbili baina yake na Yanga unavyoenda kutokuwa sawa.
0 COMMENTS:
Post a Comment