WAWA AWAJIBU NAMNA HII WALIOPONDA KIWANGO CHAKE KAGAME
Beki wa kati wa Simba, Pascal Wawa amewashangaa wanaodai uwezo wake umefikia mwisho na wala hana hofu kama Simba itaamua kumtema kwani bado anaamini kiwango chake kipo juu.
Beki huyo ambaye licha ya kutambulishwa na uongozi wa timu hiyo lakini inaelezwa hajasaini mkataba wowote kwa kuwa alipewa nafasi ya kujaribiwa katika michuano ya Kombe la Kagame iliyomalizika hivi karibuni.
Kwa mujibu wa gazeti la championi, Wawa alisema kuwa kwa upande wake hana wasiwasi wowote iwapo Simba itaamua kumuacha kufuatia madai ya kutokuwa na kiwango kama inavyodaiwa na baadhi ya mashabiki.
“Kiukweli hilo jambo limenishtua, akina nani wanasema nimeisha uwezo wa kucheza mpira na kwa nini, hao hawajui wanachokisema hawajui chochote mimi bado nipo sawa na uwezo wangu haujashuka wala nini.
“Sina cha kuhofia najua wapi nimetoka na uwezo wangu upoje hata uongozi ukiamua kuniacha sina hofu ni sawa tu kwa sababu Mungu ndiyo anajua kila kitu na siku zote nimekuwa nikimuamini yeye tu.
HABARI HII COPY AND PASTE
ReplyDelete