DEMBELE, MAGUIRE, MOURINHO, MANCHESTER UNITED, ARSENAL: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO
Mlinzi wa Leicester na England Harry Maguire bado ana matumaini kuwa anahamia Manchester United ambayo ofa zake mbili tayari zimekataliwa na mchezaji huyo mwenye miaka 25. (Sky Sports)
Nao Leicester wana nia ya kumuuza Maguire kwenda Manchester United. (Daily Mail)
Naye meneja wa Manchester United Jose Mourinho ana wasiwasi klabu hiyo itakosa kumsaini mchezaji yeyote kabla ya siku ya mwisho leo Alhamisi. (Times)
Arsenal wanatathmini hatua za mwisho kumwendea mchezaji raia wa Croatia Domagoj Vida baada ya kuambiwa kuwa watalipa pauni milioni 26.9 kumsaini mchezaji huyo mweye miaka 29 mlinzi wa Besiktas. (London Evening Standard)
Arsenal wanaweza kutumia pauni milioni 10 kwa mkopo wa msimu wote kwa mshambuliaji wa Barcelona mwenye miaka 21 Mfaransa Ousmane Dembele, wakiwa mpango wa kulipa pauni zingine milioni 90 ili mchezaji huyo aweze kuhama kabisa msimu ujao. (Mundo Deportivo, kupitia Football London)
Manchester United wamemkosa mlinzi wa Bayern Muninch raia wa Ujerumani mwenye miaka 29 Jerome Boateng kwa sababu walikuwa wanamtaka kwa mkopo tu. (Sun)
Boateng amekubali kujiunga na klabu ya Ufaransa ya Paris St-Germain, huku Bayern wakijiandaa kumuuza kwa pauni milioni 40.5. (Le Parisien)
Mchezaji mwenye umri wa miaka 22 wa Aston Villa na kiungo wa kati wa England Jack Grealish hajakata tamaa ya kujiunga na Tottenham kabla ya tarehe ya mwisho, licha ya klabu yake kuzuia kuhama kwake kwa gharama ya pauni milioni 25. (Sky Sports)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment