Mshambuliaji Mtanzania, Thomas Ulimwengu sasa amerejea katika kiwango chake baada ya kupiga mabao manne katika mechi saba alizoichezea timu yake ya Al Hilal Omdurman ya Sudan.
Ulimwengu amefunga mabao manne huku akitoa pasi moja yaani asisti iliyozaa bao katika mechi hizo saba.
Hii inamfanya Ulimwengu kuwa mmoja wa wachezaji gumzo katika ligi hiyo ambayo ni moja ya ligi kongwe barani Afrika.
Ulimwengu amejiunga na timu hiyo maarufu na moja ya klabu tajiri barani Afrika akitokea AFC ya Sweden ambako alilazimika kukaa nje kwa muda kutokana na majeruhi.
Lakini tokea amerejea dimbani, Ulimwengu amekuwa moto mkali kwa mabeki wa Ligi Kuu Sudan.
Kabla Ulimwengu alifanya vizuri akiwa na TP Mazembe ya DR Congo na kufanikiwa kuweka rekodi kadhaa ikiwemo kubeba ubingwa wa Afrika na kuwa mmoja wa Watanzania waliocheza Kombe la Dunia la Klabu.
0 COMMENTS:
Post a Comment