ITC imemfanya Chama kukosa mechi tatu ambazo ni dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Ngao ya Jamii, dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City katika Ligi Kuu Bara.
Kiungo huyo fundi aliwasili nchini kujiunga na Simba baada ya mabosi wake kumalizana na Dynamo FC ambayo alikuwa akiichezea huko Zambia.
Ujio wa ITC hiyo utamfanya Chama sasa kuanza kazi take rasmi ndani ya wekundu wa Msimbazi akiungana na Deogratius Munish 'Dida' ambaye tayari naye ITC yake imeshawasili.
Chama ataanza kibarua chake cha kwanza kuichezea Simba dhidi ya Lipuli, mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.








Haifai..
ReplyDeleteHatriiiiii
ReplyDeleteMe Bado siamini mpaka aseme Manara maana hii blog mnatulisha sana matango poli mpaka kikosi kinachoanza pia mnadanganya?
ReplyDeletehivi simba imecheza mechi ngapi za ligi
ReplyDeleteSaleh Ally uwe makini na uandishi wako. Pamoja na kwamba wewe ni binadamu lakini unapoona makosa ya kiuandishi uwe una edit. UTC na ITV ndiyo nini?
ReplyDelete