August 22, 2018


Mwanamuziki mkongwe kwenye Tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ hivi karibuni mbele ya umati wa mashabiki alizua gumzo kutokana na kauli yake kwamba hana mpango wa kuoa.

Dully alifunguka suala hilo wakati akiwa jukwaani akikamua kwenye Tamasha la Komaa, lililofanyika kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, ambapo akiwa katikati ya shoo alisema kwa nguvu; “Dar es Salaam…hatupoi… hatuboi na wala hatuoiii…”

Baada ya kauli hiyo swangwe ziliibuka kila kona na baadhi ya mashabiki walianza kuzungumza chini kwa chini juu ya kauli hiyo kwamba huenda Dully hana mpango wa kuoa kweli ndiyo maana kasema juu ya kauli hiyo. Hata hivyo mara kadhaa Dully amekuwa akiulizwa juu ya kuoa na kutoa majibu yasiyonyooka, akidai wakati wake wa kuoa ukifika watu watafahamu na wasiwe na haraka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic