August 21, 2018




Pamoja na wengi kuonekana hawampi heshima ya mchango wake katika mchezo wa soka, Kocha Arsene Wenger amepewa tuzo yenye heshima ya Rais.

Tuzo hiyo yenye heshima ya juu imetolewa na Rais wa Liberia, George Weah ambaye amemtunuku Wenger kwa mchango mkubwa.

Tuzo hiyo itatolewa rasmi Ijumaa kwa Wenger.

Wenger ndiye aliyemtambua Weah kwa mara ya kwanza hadi kumpa nafasi ya kuichezea AS Monaco ya Ufaransa, yeye akiwa kocha mkuu.

Baadaye, Weah alikwenda na kuwa nyota zaidi Afrika hadi aliposhinda tuzo ya mwanasoka bora wa dunia akiwa na AC Milan.

Hadi sasa, Weah anashikilia heshima ya kuwa mwanasoka bora duniani akitokea Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic