KIBALI CHA ZAHERA YANGA BADO NI PASUA KICHWA, UONGOZI WATOA TENA TAMKO
Na George Mganga
Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili, Hussein Nyika, umesema bado unapambania kibali cha Kocha wake Mkuu, Mwinyi Zahera.
Nyika amesema mpaka sasa kibali cha kazi nchini ambacho Zahera anapaswa kuwa nacho hakijapatikana hivyo juhudi zinaendelea ili kufanikisha na hatimaye awe anakaa kwenye bechi la ufundi wakati wa mechi.
Kiongozi huyo ameeleza kuwa kibal hicho kitapatikana kwa kushirikiana na serikali na mpaka sasa wanaendelea kupambana ili kiweze kupatikana.
Kelekea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika Agosti 29 dhidi ya Rayon Sports itakayopigwa huko Rwanda, uongozi umeeleza kuwa wanahangikia kukipata kibali ili ikiwezekana Zahera akawe sehemu ya benchi la ufundi.
Tangu kuwasili kwa Zahera nchini ambaye amechukua mikoba ya Mzambia, George Lwandamina, mpaka sasa hajafanikiwa kupata kibali hicho na akiwa ana miezi takribani mitatu hapa nchini.
Tatizo hasa ni nini mbona kila siku mnazungusha tu? mara umbali kati ya dar na dodoma hasahasa nini kinachelewesha kama malipo tuambiwe tuongeze michango.
ReplyDeleteKama hamuwezi tafuteni watu msaidiwe, hii kazi imewashinda
ReplyDeleteYangi inaamini wanaweza kufanya kitu wenyewe na huona aibu kutaka misaada na huku timu nyenginezo zinapata vibali. Bila ya shaka kuna pingamizi fulani lakini wanaona aibu kuliweka wazi na huku wamegeuka sabuni wanayeyuka kidogokidogo. Kwa anafika Simba anafika leo kesho kila kitu tayari
ReplyDelete