August 22, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuanza kwa kasi kuonesha makucha yake ndani ya kikosi cha Simba, kiungo mpya aliyesajiliwa kutokea Mtibwa Sugar, Hassan Dilunga, amesema ndoto zake ni kucheza soka Ulaya.

Kiungo huyo fundi aliyechukua namba ya Mzambia kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Sugar, Clatous Chama ambaye mpaka sasa hajapata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) , anaamini kupitia Simba atasonga mbele zaidi.

Dilunga ameeleza kuwa anaamini kama atapambana akiwa Simba anaweza akatimiza ndoto kupitia Simba endapo atazidi kupambana zaidi ili kutimiza adhimio lake.

Wakati mchezaji hajasajiliwa na Mabingwa hao wa Soka hapa nchini kwa msimu wa 2017/18, awali ilikuwa ikielezwa kuwa mabosi wake wa zamani Yanga walikuwa wakimuwinda.

Dilunga alifanikiwa kutua Simba kwa kusaini kandarasi ya muda wa miaka miwili ambayo itaisha mwaka 2020.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic