August 22, 2018


Na George Mganga

Kuelekea kufunguliwa kwa pazia la michuano ya Ligi Kuu Bara leo, uongozi wa klabu ya Simba umeendelea kutamba juu ya kuingia idadi ya mashabiki wengi viwanjani.

Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Habari wa klabu, Haji Manara, akisema kuwa wapenzi, mashabiki pamoja na wanachama wa klabu hiyo watazidi kumiminika kwa wingi zaidi.

Manara ameeleza kuwa Simba ndiyo imeshika rekodi hiyo kwa kuingiza mashabiki wengi pale inapocheza pamoja na mapato huku ikiweka rekodi hiyo katika msimu uliopita.

Kutokana na kuweka rekodi hiyo, Manara amezidi kuwaomba mashabiki wa timu hiyo kuzidi kujitokeza kwa wingi ikiwemo leo ambapo kikosi cha timu hiyo kitafungua rasmi pazia la ligi kwa kucheza na Tanzania Prisons ya Mbeya.

Simba itaingia kucheza na Prisons majira ya saa moja kamili usiku ukiwa ni mchezo wake wa kwanza kwa ajili ya kuanza kutetea mbio za ubingwa.

1 COMMENTS:

  1. Tatizo hata wakijitokeza kwa wingi mikoani huna chako manara

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic