August 14, 2018


Heritier Makambo ndiye mchezaji gumzo zaidi katika kikosi cha Yanga na huenda atawavuta mashabiki wengi zaidi wa klabu hiyo wakati timu hiyo itakapocheza jijini Dar es Salaam.

Yanga itacheza dhidi ya USM Alger Jumapili kwenye uwanja huo na mashabiki wengi wa Yanga wameonekana wanataka kuiona kazi yake.

Makambo raia wa DR Congo ambaye amejiunga na Yanga msimu huu amekuwa gumzo kutokana na kufanikiw akufunga mabao mawili katika mechi za kujipima kujiandaa na msimu mpya.

Lakini kwa kuwa Yanga imeondokewa na washambulizi wake kama Donald Ngoma huku waliopo kama Amissi Tambwe wakionekana kushuka kutokana na kuandamwa na majeraha, Makambo amekuwa ndiye gumzo zaidi.

Katika makundi mbalimbali ya mitandao ya kijamii, SALEHJEMBE imeshuhudia Makambo akiwa ndiye gumzo zaidi kwa wachezaji wa Yanga. Wako wakiamini  atafanya makubwa na wengine wakiona ni ukali wa mwanzo akitaka kujihakikishia ajira.


Wengi wamekuwa wakisisitiza kutaka kumuona Uwanja wa Taifa ili waweze kumpima kwa usahihi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic