KUMEKUCHA JANGWANI, MANJI KUWASHUHUDIA YANGA WAKIKIPIGA NA WAARABU TAIFA
Na George Mganga
Uongozi wa Yanga umemtangaza Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga dhidi ya USM Alger utakaopigwa Uwanja wa Taifa Jumapili hii.
Yanga itashuka dimbani kucheza mchezo huo wa mkondo wa pili baada ya kupoteza ule wa kwanza huko Algiers, Algeria kwa kufungwa mabao 4-0.
Mbali na Jenerali Mabeyo, uongozi wa Yanga umesema aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mfanyabiashara Yusuph Manji, naye atakuwepo Uwanjani hapo kuishuhudia timu yake.
Manji atakuwa anarejea rasmi Uwanja wa Taifa kuitazama Yanga ikiwa ni takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu atangaze kujizulu wadhifa wake ndani ya klabu hiyo.
Uwepo wa Manji unaweza kuwa baraka na neema kwa wadau, wanachama, wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo ambayo imekuwa ikipitia kipindi kigumu hivi sasa.
Mechi hiyo itapigwa majira ya saa 1 za usiku kwa mujibu wa ratiba na itaoneshwa mubashara na kituo cha Azam TV.








ACHENI UONGO MANJI HAWEZI KUJA UWANJANI. MNATULAGHAI ILI WATU TUJE UWANJANI KISA KUMUONA MANJI MWENYEKITI WA YANGA ALIYEJIUZURU. ACHENI KUONGOPA MANJI HANA MPANGO HUO.
ReplyDeleteWewe nani yake mpk useme haji
DeleteWe boya kweli.....kwani we mkewe kwamba ndo umemshauri asije uwanjani au?,by the way hatuendi uwanjani kwa sababu ya manji......tunakwenda kuangalia soka na tulishapanga hivyo kabla hata hawajatangaza kuwa manji atakuwepo.
ReplyDeleteHahahahahaha
ReplyDelete