WEKUNDU WA TERMINAL WAING'ARISHA STAND YA MABASI UBUNGO
Tawi la klabu ya Simba Ubungo linalojulikana kwa jina la Wekundu wa Termina, jana limesafisha eneo linalozunguka kituo cha mabasi ya ubungo ikiwa ni wiki ya Simba kuelekea Simba Day.
Msemaji wa tawi hilo, Masoud Chike, amesema wamemua kufanya tukio hilo ili kuonesha upendo eneo wanalokaa na zikiwa zimesalia siku 3 pekee kuelekea tamasha la Simba Day.
Chike ameeleza tawi hilo limefanya usafi kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa Simba ambao wanatokea katika kitengo cha kamati ya Utendaji.
Aidha, Chike amesema tawi na Wekundu wa Terminal litapata nafasi ya kukutana na kikossi cha wachezaji wa Simba Agosti 7 ikiwa imesalia siku moja pekee kuelekea tamasha hilo kubwa.
Mwenyekiti huyo amesema lengo kubwa la kukutana na wachezaji ni kuweza kubadilishana mawazo pia kutiana morali kuelekea tamasha hilo ambalo Simba itacheza dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana.
0 COMMENTS:
Post a Comment