Mshambuliaji mpya hatari hivi sasa wa Yanga, Mkongoman, Heritier Makambo, ametoa pongezi kwa viungo wa timu hiyo, Feisal Salim ‘Fei Toto’ na Papy Tshishimbi ambao ndiyo wana siri ya mabao yake anayofunga.
Kauli hiyo, aliitoa ikiwa ni saa chache baada ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar kumalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-1 juzi Alhamisi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mkongomani huyo hivi sasa amepata umaarufu mkubwa katika msimu huu kutokana na kasi yake aliyoanza nayo ya kufunga mabao, pia uwezo wake wa kupambana na mabeki wa timu pinzani ambapo tayari amefunga mabao sita.
Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Makambo alisema pongezi nyingi ziende kwa viungo wake hao ambao wamekuwa wakifanya kazi kubwa na nzuri ya kumtengenezea mabao.
Makambo alisema, kama viungo hao wakiendelea kucheza pamoja kwa muda na kuzoeana, basi ana matarajio makubwa ya kufunga mabao mengi kutokana na aina ya pasi wanazompatia.
“Pongezi nyingi ziende kwa viungo wangu wachezeshaji Fei Toto, Tshishimbi, Raphael (Daudi) na wengine ambao wamekuwa wakitimiza majukumu yao ya kunichezesha, kwa maana ya kunipigia pasi na krosi nzuri za kufunga mabao.
“Ukiangalia mechi (dhidi ya Mtibwa), utaona kazi kubwa iliyofanywa ya viungo wakabaji na wachezeshaji ambao walitutengenezea nafasi nzuri za kufunga mabao, pia kupunguza mashambulizi kwa maana ya kukaa na mipira kwa lengo la kutoipoteza.
“Ni matarajio yangu kuona viungo hao wakiendelea kutimiza majukumu yao kwa faida ya timu katika kuwapa furaha mashabiki wetu wa Yanga kwa kupata matokeo mazuri,” alisenma Makambo.
0 COMMENTS:
Post a Comment