August 28, 2018


Wakati kikosi cha Yanga kikiwa jijini Kigali, Rwanda tayari kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports, timu hiyo imewaacha nyota wake kadhaa nchini.

Kikosi hicho kimeenda na msafara wa watu 25 ukiwa na wachezaji 17 pamoja ba viongozi 8 huku majina kadhaa yakibakia Dar es Salaam kwa sababu mbalimbali.

Wachezaji hao ni Said Makapu, Juma Mahadhi, Thaban Kamusoko, Papy Tshishimbi, Haji Mwinyi, Juma Abdul na Amis Tambwe.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka Yanga zinasema Abdul na Mahadhi wamesalia Dar es Salaam kwa vile ni majeruhi huku Tambwe na Kamusoko wakikosa vibali vya mchezo huo.

AIdha, uongozi umesema Makapu amesalia kutokana na kupatwa na msiba huku wengine wote tajwa hapo juu wakiwa ni majeruhi.

Yanga itashuka kucheza na Rayon Agosti 29 kesho ikiwa mkiani kwenye Kundi D baada ya kushinda mechi moja pekee na suluhu moja.

Katika mchezo wa awali ambao Yanga ilicheza dhidi ya Rayon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, iliweza kwenda suluhu ya bila kufungana na kesho watacheza mechi ya mkondo wa pili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic