August 30, 2018


Mama mzazi Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi, Bi. Desderia aliyefariki dunia katika Hospitali yaTaifa ya Muhimbili, amezikwa jana nyumbni kwake maeneo ya Sai, Kwa Mbilinyi, jijini Mbeya.

Akizungumza katika Mazishi hayo, Mbowe amesema Chama chao kinapitia katika wakati mgumu kutokana na viongozi hao kukabiliwa na kesi katika mahakama mbalimbali nchini kwa tuhuma tofauti tofauti huku akiwasisitiza wakazi wa Mbeya kushikamana na kuwa wamoja.

“Kufungwa kwa Sugu na Masonga ilikuwa ni ishara ya kuuona ufalme wa Mungu. Viongozi wanashatakiwa, wengine wanafungwa, wengine wanauawa, na wengine wanapigwa risasi, huu ni wakati wa kuonyesha umoja wetu,” alisema Mbowe.

“Natambua mama aliumia sana ulipofungwa kwa kuonewa pale gerezani, lakini hii iwe ni mbegu ambayo itakusaidia uote, ukasimame katika haki kuitetea demokrasia ya nchi hii, kuhakikisha haki za watu zinalindwa, uhuru wa mawazo, kama Mungu ambavyo alituweka hapa duniani sote tuheshimiane kwa sababu sote ni watu wa muhimu katika dunia hii,” alisema Mchungaji Peter Msigwa (Mb).

Mama wa Sugu alifariki dunia Agosti 26, mwaka huu na kwa mujibu wa Sugu mwenyewe, mama yake alianza kuumwa baada ya Sugu kufungwa jela Februari 26, mwaka huu.


2 COMMENTS:

  1. Kiasi fulani upinzani una kila dalili ya kuishiwa hoja na kuanza kutumia misiba kama majukwaa ya kisiasa yaani hovyo kabisa. Ukichunguza siasa za Chadema ni za kijinga. Huwezi kuvunja sheria za nchi eti kwa sababu ni chama kikuu cha upinzani nchini halafu serikali ikae kimya bila ya kuchukua hatua yeyote.

    ReplyDelete
  2. Alafu uliyetoa post hapo juu mungu anakuona kwahiyo sheria wanavunja watu Fulani Tu wengine hawavunji kwahiyo mbunge kupigwa risasi naye sababu ya kuvunja sheria na hukumu yake kupigwa risasa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic