August 30, 2018


Kiungo mpya wa klabu ya Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto', amesema kuwa alichelewa kujiunga na kambi ya Taifa Stars baada ya kwenda kwenye msiba wa mchezaji mweziye, Said Makapu.

Toto alikuwa Zanzibar kwa ajili ya kumpa pole Makapu ambaye lifiwa na mama yake jamb ambalo lilipelekea akaondolewa kwenye msafara wa wachezaji waliosafiri kuelekea Rwanda kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports.

Kiungo huyo aliondolewa kwenye kikosi cha Stars kwa sababu alichelewa kuripoti kambini, jambo ambalo TFF imelichukulia kama utovu wa nidhamu.

Toto anakuwa katika ile orodha ya wachezaji 6 wa Simba ambao waliondolewa pia baada ya kuchelewa kambini bila kutoa taarifa ya sababu za wao kufanya hivyo.

9 COMMENTS:

  1. Yuko sahihi Fei Toto kosa lake kutokutoa taarifa nadhani kama angetoa taarifa sidhani kama yangetokea yaluyomkuta

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli hakutoa taarifa hill ni kosa ,je hao viongozi wamemuuliza tatizo ni nini kabla ya kumuengua?

      Delete
  2. Haina shida Tanzania tuna lundo la wachezaji yeyote akivaa jezi ya taifa atacheza vizuri tuu hata hawa waliopo kambini TFF ikitaka fukuza wotee tutapata timu nyingine nzuri tu na tutashinda. TFF safiiii?

    ReplyDelete
  3. TFF itakosea kabisa kisongizio kila ayatakayo kocha kwakuwa yeye ndie mwalimu mkuu. Walimu au viongozi daima hukosa na kukosolewa au kutumbuliwa. Si tumeona viongozi wa ngazi za juu ama wametumbuliwa au kunyanganwa vyeo wakiwemo mawaziri, wakuu wa mikoa na wawilaya pamoja na wakurugenzi na wengi hapahapa nyumbani na kwengineko kufika hadi kuonywa na kuwachishwa kazikazi. zNi kosa kubwa au udhaifu kwa viongozi eti kuunga mkono kuenguliwa na kufukuzwa kabisa kuitumikia taifa kwa karibu tuwi au uti wa mgongo karibu wachezaji wote kwa kocha ambaye uwezo wake haujulikani na hata ikiwa anao uwezo asiachiwe kufukuza wenye uwezo mkuu. Kubomoa ni rahisi sana lakini kujenga ni vigumu ulichokijenga kwa miaka unaweza kukibomowa kwa saa tu na pindi hata wachezaji hao waliofukuzwa wakihitajiwa tena watakuwa na imani na kocha huyo au wale waliouunga mkono kutimuliwa kwao au ndio keshaamuwa kuwafukuza once and for good.

    ReplyDelete
  4. wangewahoji Kwanza kabla ya kuwaadhibu, hiyo ni taasisi. sidhani Kama mtoto akikosa anaadhibiwa bila kujua sababu yake

    ReplyDelete
  5. Kocha atatengeneza magroup,tutarajie kuwepo kwa watanzania kushangilia uganda

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hao watanzania wa kushangilia uganda watakuwa ni baadhi ya wanasimba wasio na weledi,sisi yanga tumeridhika na maamuzi ya kocha hata kama mchezaji wetu feisal nae yumo......nidhamu ndo kila kitu,tusilee upumbavu na utovu wa nidhamu.

      Delete
  6. Enter your comment...kuna watu wanaandika yaani unasoma hadi unakuchoka

    ReplyDelete
  7. Ili utengeneze timu lazima nidhamu iwe ndio kipaumbele. Watanzania tumezoea kukumbatia uozo. Wachezaji wamepewa taarifa na muda wa kuripoti kambini sasa nini kuwatetea. Unataka kuitengeneza timu ya Rashid Yekin alafu una wachezaji ambao hawajitambui na kujua umuhimu wa Taifa. Hao wote fukuza...tutatengeneza timu yenye discipline kuanzia ndani ya uwanja hadi nje ya uwanja. Hata Misri hamjaanza kucheza na wala hamuhitajiki mmeanza kuvimbisha makwapa. Timu ikikosa nidhamu nje basi ujue hadi ndani ya uwanja watakuwa vivyo hivyo. Kihimbwa, Kiduku, Kimenya, Dumayo na wengine walioitwa wana uwezo wa kufanya vizuri kuliko hao ambao mnawatetea. Hata wakikosa lakini hawa wanauwezo wa kwenda kuchukua nafasi zao. Timu itakuwa hivi:-

    1) Manula
    2) Kesy
    3) Gadiel
    4) Mwantika
    5) Calvin
    6) Himid
    7) Farid Musa
    8) Dumayo
    9) Samata
    10) Ulimwengu
    11) Kihimbwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic