MCHEZAJI SIMBA AAMUA KUIKACHA TIMU YAKE
Kiungo Mkongwe Mwinyi Kazimoto, amewaaga rasmi mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba kwa kipindi chote ambacho ameichezea timu hiyo.
Kazimoto ametoa shukrani zake kwa wanachama na mashabiki wa Simba kutokana na mchango ambao ameupata kutoka kwao kwa muda huo wote aliofanikiwa kukipiga Msimbazi ikiwa ni baada ya kuachana rasmi na timu hiyo.
Kazimoto amesema kwa sasa ameamua kujiunga rasmi na JKT Tanzania ambayo imepanda daraja kushiriki Ligi Kuu Bara.
"Asante kwa mashabiki, wanachama na wapenzi wa simba kwa kipindi chote nlichokua hapo mlikua namiminyakati zote,tulilia pamoja na kucheka pamoja"
Lakini kila kitu kina mwisho, nashukuru kwa muda wote niliokuwepo klabuni, maisha ya mpira ni safari naanza maisha mapya ndani ya klabu yangu mpya (JKT), muwe na wakati mwema" alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment