August 6, 2018


Everton wamefikia makubaliano na Barcelona kumsaini mlinzi wa Colombia Yerry Mina, 23, kwa pauni milioni 28.5 kwa mkataba wa miaka mitano. (Sport - in Spanish)

Everton wamewaambia Manchester United kuwa watamchukua beki ya miaka 28 raia wa England Chris Smalling au mlizni wa Sweden Victor Lindelof, 24, ikiwa klabu hizo mbili hazitaafikia makubaliano kuhusu mlinzi raia wa Argentina Marcos Rojo, 28. (Teamtalk)

Manchester United wanajiandaa kutoa ofa kwa beki wa Leicester Harry Maguire, 25, na kwamba sasa wanaweza kulipa pesa nyingi zaidi katika rekodi kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England. (Sky Sports)

Wakati huo huo Manchester United wamefanya mawasiliano na Bayern Munich kumsaini mlinzi mwenye miaka 29 mjerumani Jorome Boateng kwa kima cha pauni milioni 44.5. (Bild - in German)

Chelsea wako katika nafasi nzuri kumsaini kwa pauni milioni 75 wing'a wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 25, baada ya Tottenham kujiondoa. (Mirror)

Ofa ya Leicester ya pauni milioni 10 imekataliwa kwa mlinzi wa Brentford Chris Mepham, 20, huku nao Bournemouth wakimmezea mate mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales. (Mail)

Wolves wanataka kuilipa Middlesbrough pauni milioni 22 kwa awamu kwa wing'a raia wa Uhispania Adama Traore, 22, badala ya malipo yote kwa jumla kwa kulipa kwanza paunia milioni 18. (Sun)

Crystal Palace wako kwenye mazungumzo kumsaini mshambuliaji wa Red Bull Salzburg raia wa Israel Munas Dabbur, 26. (Mail)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic