May 10, 2019


KIKOSI cha Azam FC Jana kilitoshana nguvu na kikosi cha KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Chamazi majira ya saa 1:00 Usiku.

Suluhu hiyo inawafanya wajikusanyie pointi moja na kubaki nafasi ya tatu wakiwa na pointi 68.

Mratibu wa Azam FC amesema kuwa kwa sasa ratiba imekuwa ikiwabana licha ya kujiaandaa vizuri kwani kwa sasa ratiba yao ni bandika bandua kila baada ya kumaliza mchezo unafuata mchezo mwingine baada ya kuacha pointi tatu kwa Yanga.

"Tumetoka Shinyanga,ambapo tulicheza na Stand United, hivyo mazoezi yetu kuivaa KMC tumefanya juzi jioni, hivyo bado tuna kazi ngumu ya kufanya.

"Kwa sasa ni bandika bandua, tumemalizana na KMC, tuna mchezo mwingine Mei 13 dhidi ya Simba tena nao utakuwa ni mchezo mgumu lakini tupo tayari, mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema Alando.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic