September 13, 2021

 


BAADA ya kikosi cha Yanga kupoteza katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United,  uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kuwa bado una nafasi ya kupata matokeo katika mchezo wa marudio.


Katika mchezo uliochezwa jana Septemba 12, baada ya dakika 90, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 0-1 Yanga jambo lililowapa maumivu mashabiki pamoja na Watanzania kiujumla.


Bao pekee la ushindi lilipachikwa na Moses kwa kichwa akiwa ndani ya 18 baada ya kipa namba moja wa Yanga, Diarra Djigui kutoka kidogo katika eneo lake.

Haji Manara,  Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa kuna dakika 90 za kupambana.

"Tunazo dakika 90 nyingine za kupambania timu yetu, chini ya jua hili hakuna kisichowezekana. Tupeane pole kwa matokeo lakini tusikate tamaa," 


Katika mchezo wa jana Septemba 12 rekodi zinaonyesha kuwa Yanga ilipiga jumla ya kona 7 huku Rivers United wakipiga kona moja na Yanga ilipiga jumla ya mashuti 13 na ni moja lililenga lango huku Rivers United ikipiga mashuti 11 na ni mawili yalilenga lango.

Kibarua kikubwa ni kwenda kushinda mabao zaidi ya mawili kwa sababu wapinzani wao wanafaida ya bao la ugenini.

Mchezo wao wa marudi unatarajiwa kuchezwa Septemba 18 nchini Nigeria na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa hakuna mwenye uhakika wa kusonga mbele kwa wakati huu mpaka dakika hizo 90 zitakapomeguka.

17 COMMENTS:

  1. Yanga wamesema kuwa hawakupata matayarisho stahiki na ndio sababu ya kupoteza. Walikuwepo Moroco siku kadha na kurejea kwa sababu zisizo na msingi lakini wakasema wamefaidiks na baada ys kurejea wakaingia kambini na siku zote wakijinasibu kuwa wamefaifika na wapo tayari kwa makombe yote na kutokana na mazowezi hayo wanahakikia watawashinda Rivers kwa magoli mengi na mkwanja wa bilioni upo mezani lakini leo tunsikia hawakupata mazowezi mazuri

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli bado walihitaji muda zaidi. Kuna timu zina miezi 2 ya matayarisho. Naona muda mwingi unapotea kwenye mchakato wa usajili kitu ambacho lazima kirekebishwe ili kutoa muda zaidi we matayarisho kama wenzetu wa Zambia, Nigeria na nchi nyingine.

      Delete
    2. kuna sababu ya msingi ya kubadili nusu ya kikosi mlichokuwa nacho mwaka jana..hamjifunzi kila mwaka msimu ukianza mbili ya tatu ni wapya. kuna kilichowazuia kuanza maandalizi miezi miwili iliyopita ?

      Delete
    3. Mabadiliko wamefanya ila Ni ya MSEMAJI!

      Delete
    4. WATU wengine hushindwa kuelewa.
      YANGA KUSAFIRI KWENDA MOROCCO ILIKUWA KWA ajili ya kuiga SIMBA KWASABABU NI MUDA MREFU SANA YANGA HAWAJAPANDA NDEGE KWENDA NJE YA NCHI!

      NDIO MAANA WALISEMA WAMEFAIDIKA.

      KUNA WAVHEZAJI HUWA HUPATA MSONGO WA MAWAZO MFANO KARINYOS WALIMPOKEA KWA SHANGWE UWANJA WA NDEGE WAKATI WA KUONDOKA KAONDOKA KIMYAAAAA!

      Delete
  2. Yanga kwa matamko wapo vizuri ila uwanjani kimeo 😂

    ReplyDelete
    Replies
    1. YANGA wana AKILI Maana wamesajili MSEMAJI badala ya TIMU nzuri .ili Baadaye wasajili wachezaji .
      that is Good! Hatua kwa Hatua watafika Kigoma Na kushinda.

      Delete
  3. The Return of the UTOPOLIONS

    ReplyDelete
  4. Na wale mliowapa corona fake nao wasemeje?tena wale key players ndio mkaona muwape corona,sasa subirin mfike nigeria muone kama na nyie hamtapewa corona first 11 yote na mechi lazima ichezwe.kila mla cha mwenzie na chake lazima kiliwe,mungu hataki zambi mmefungwa vivyo hivyo jumlisha na laana za aliyewabeba alafu hamtaki kuwashimu,YANGA tambua kwamba unapaswa kumuheshimu aliyekufanya ukafika hapo ulipo,kama sio simba usingecheza kimataifa ila tambua pia kama sio laana ungeshinda jana,utaendelea kuteseka sana bado

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani Yanga ndio wanaowapima? Makoro sifa yenu kubwa ni midomo mirefu kama chupa

      Delete
  5. Majibu yao ni maneno ya ovyo ovyo bila ya mpangilio

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndivyo walivyoumbwa hao,usiwalaumu,chamsingi waombeen sana labda watabadilika.ila ukweli ni kwamba hawana shukurani.

      Delete
  6. Tatizo sio kubwa lipo kwa hao viongozi kuwaacha baadhi ya lundo la wachezaji kibao hiyo ndio faida yake we kila msimu ni kutoa wachezaji 8+ una nunua wachezaji 14 inategemea utapata timu iliyo bora hapo chamsingi ni kutoka kwenye mashindano na kujipanga upya next time ndionwaje ss kamili kwenye hayo mashindano it's so sad timu kama Yanga kukwama mwanzoni tu

    ReplyDelete
  7. Wallace karia na bodi zake wanajua wanachofanya, huwez maliza ligi kuu bara mwez wa nane halafu wa tisa unaanza ligi ya mabingwa, usajil lini, mapumziko lini, matayariso lini,
    Tuangalie tar 25 simba vs yanga kigoma, mapumziko yakaanza, waoe wiki 1 kupumzika baada ya kaz kubwa ya miez kadhaa. tangu agost 2 hadi jana ni takriban week 6 hapo usajiri, training na friend match.
    Hata ingekuwa ww usingeweza mambo muhimu matatu yafanikiwe ndan ya mwez mmoja..
    Ndan ya mwez huo kuna mechi za kitaifa, kombe la dunia...
    Wenzetu tangu julai mwanzoni walikamilisha ligi wana miez miwil ya maandaliz na likizo, leo uje uwalinganishe.
    Kwetu huku wallace viporo kila leo, kuahirisha mechi ni kama sambusa tu.

    ReplyDelete
  8. YANGA imemsajili msemaji badala ya mchezaji!
    By Komandoo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic