August 21, 2018


Kocha Mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera ameibuka na kusema wao na Simba hawana utofauti kutokana na mafanikio ya kambi ya Morogoro.

Jeuri hiyo imekuja kufuatia kuwalaza Waarabu mabao 2-1 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger kwenye Uwanja wa Taifa juzi.

Zahera anaamini kuwa wao Simba na Azam wana usawa kutokana na kikosi chake kuimarika tofauti na hapo awali kupewa nafasi finyu ya kufanya vema kuelekea Ligi Kuu Bara msimu ujao.

"Tulikuwa na wiki mbili za mazoezi Morogoro kwa sasa timu ilivyo naweza kusema tunaweza kuwa katika usawa na timu zingine kama zile zilizoenda Uturuki na hata Uganda katika ubora''

''Timu sasa imeimarika nafurahi tuna kikosi imara cha kushindana na timu yoyote, wachezaji tuliowaongeza wameleta nguvu na ukiongeza na hawa waliokuwepo timu yetu ipo vizuri" alisema.

14 COMMENTS:

  1. Hiyo timu ya Al Jeria iliyofungwa na yanga nayo pia hivi karibuni ilopoteza mchezo

    ReplyDelete
    Replies
    1. alifungwa kwenye mashindano gani?......fafanua,usiongee kwa wivu.

      Delete
  2. Kwa kweli kwa mechi ya juzi dhidi ya waarabu, sisi kama yanga tumefunga timu nyng xna ndani ya hiyo mechi moja. Kwanz tumempiga usm alger, tumempiga simba(mwny ubingwa wetu) na mtibwa. Nakaribisha usajili wa mashabiki wanaotaka kurudi yanga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mika kwani kuna mashabiki waliondoka Yanga?..Halafu Simba na Mtibwa mmewafungaje.Kwa hiyo unataka kusema mlivyopigwa 4 kule Algeria mlifungwa pia na Simba??..

      Delete
  3. Timu iko vzr cha muhimu tu wachezaji wtu waendelee kujituma kila mechi, naamini ubingwa ni wtu

    ReplyDelete
  4. Kuchonga sana hakufai jamani. Nimeona hata kocha wa mtibwa nae anachonga kuwa wao na simba wapo sawa kimchezo. Hata msimu uliopita Simba ilibezwa kwa kuweka kambi Africa kusini lakini mwisho wa siku ilikuja kuoneka nani alijiandaa vyema kwa mikiki ya ligi. Simba imejiandaa kwa mashindano ya nje na ya ndani kuthibitisha hayo ni ule upana wa kikosi chao amabacho kimejaa wachezaji wa viwango.kama Mtibwa itashiriki mashindano ya kimataifa basi kazi wanayo kwani ligi ya timu 16 mtibwa iliakata pumzi njiani sasa hii ligi ya timu 20 ukijumlisha mechi za kimataifa kwa kocha mweledi hawezi kuieka mtibwa kwenye mizani sawa na Simba katika suala la maandalizi bila ya kuchunga ulimi wake. Kuhusu Yanga ilikuwa lazima washinde ili kurejesha utulivu na matumaini isipokuwa ushindi wa mechi moja sio kuanza kuropokwa hovyo. Timu kama Azam na Simba kwa sasa zinaweza kufanya lolote watakalo hasa katika suala la motisha kwa wachezaji kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mechi zao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwisho wa siku ni Simba ndio iliyoibuka na ushindi hivyo simuelewi kocha wa Mtibwa kuwa wao na Simba wako sawa kivipi?

      Delete
    2. sasa kocha wa mtibwa alikosea nini kusema mtibwa iko sawa na simba kwa uwezo?.....ukweli si tuliuona uwanjani?,au kwa kuwa mlishinda ndo kigezo kuwa uwezo wenu ni mkubwa kuliko wao!!!!!!

      Delete
    3. Ndungulu,ukweli gani uliuona uwanjani,Simba ilishinda mechi na ilimiliki mpira pia zaidi ya Mtibwa,hicho cha Mtibwa kuwa sawa na Simba ni kwenye nini sasa

      Delete
  5. Ligi kwani inanza lini si kesho tuuuu?

    ReplyDelete
  6. Kocha weka akiba ya maneno na acha ushwahili...Pambana na hali ya timu yako na sio kuangalia timu zingine zinafanya nini ktk maandalizi yao.Kila timu ina mipangilio yake na timu za Azam na Simba zimeamua kujiendesha kibiashara hivyo kwenda nje ya Tanzania ni kuwajenga wachezaji kisakolojia kabla ya ligi na michezo ya kimataifa itakayowakabili kuanza.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utofauti atauona pale tutakapo kutana nae kwenye ligi

      Delete
  7. Ni mapema sana kutoa tahmini ya mchezo mmoja Cha msingi wachezaji waongeze jitihada uwanjani

    ReplyDelete
  8. Yanga inahitaji kujengwa kisaikoloji na kupewa motisha ili irejee kwenye makali yke kwa sasa Simba na Azam zipo juu huwezi kuzibeza

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic