August 21, 2018


Na George Mganga

Ni dhahiri shahiri Simba wameendelea na mkakati wa kuelekea kukamilisha kwa asilimia 100 mfumo mpya wa uendeshaji baada ya viongozi wa juu kuitisha kikao maalum usiku wa jana.

Kikao hicho cha Bodi ya Wakurugenzi kilichoongozwa na Mwekezaji Mohammed Dewji 'Mo' kilikuwa kinafanyika kujadili masuala mbalimbali ya klabu hiyo ambayo yatakuja kuwekwa hadharani baadaye.

Moja ya mikakati iliyojadiliwa kwenye kikao hicho ni pamoja na mbio za ubingwa kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara 2018/19.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema klabu imeamua kubadilisha mfumo huo kwa ajili ya kutomtegemea mtu mmoja na badala yake itakuwa na mwekezaji.

"Tumebadili muundo wa uendeshaji wa klabu ili kutomtegemea mfadhili, muundo huu unatupa fursa sisi na mwekezaji kuipeleke Simba mbele zaidi, shida ya kumtegemea mtu akisusa au vinginevyo ni shida"

"Sasa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi Simba kinaendelea na lolote linaloamuliwa linafanywa na Bodi na si mtu" alisema.

8 COMMENTS:

  1. Haiwezi kuwa Bodi na Makocha nao wakiwemo!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nilivyoelewa mimi Bodi ya wakuregenzi ilikutana na benchi la ufundi na ndio maana kuna agenda ya kujipanga ktk ligi ya msimu wa 2018/2019

      Delete
    2. ukiulizwa kuwa hiyo picha ni lini utasemaje? una uhakika kuwa ni picha ya kikao hicho kinachosemwa?

      Delete
  2. hiyo siyo bodi bidi inasajiliwa Brela sio kwa msajili wa vyama lazima utaalamu ufanike kutenganisha kampuni na klabu la sivyo tutachemsha. MO nani kamchagua?

    ReplyDelete
  3. Kiwango cha YANGA kimewashitua ndiyo wanaijadili kama yule babu ataweza kumdhibiti makambo kikao cha bodi akiwezi kuhusisha adi makocha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna kiwango gani pale utaisoma namba mbele ya safari

      Delete
  4. Kiwango cha YANGA kimewashitua ndiyo wanaijadili kama yule babu ataweza kumdhibiti makambo kikao cha bodi akiwezi kuhusisha adi makocha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mo ametoa pesa nyingi kwenye usajili lakini haoni kiwango kinachooneshwa na timu. Hao makocha sio muda mrefu wanafukuzwa. Mzigo wa wachezaji watabebeshwa makocha. Wachezaji wa Simba wa sasa hawajitumi hata kidogo. Kina Pawasa walikuwa hawalipwi kama wanavyolipwa hawa wa sasa lakini jitihada zao zilikuwa zinaonekana uwanjani. Tutaona mengi kwenye ligi msimu huu.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic