August 24, 2018


Baada ya kuonesha kipaji maridhawa kwa mechi kadhaa alizochezwa, imeelezwa kuwa uongozi wa Manchester United kupitia wakala wake umeanza harakati za kuwania saini ya mshambuliaji, Kelvin John anayekipiga Timu ya Taifa ya Vijana (U17), Serengeti Boys.

John ambaye yupo katika mashindano ya CECAFA na timu hiyo, aliibuka kidedea katika mchezo wa mwisho dhidi ya Rwanda kwa kufunga mabao matatu pekee katika ushindi wa mabao 4-0.

Taarifa imeeleza kuwa kigogo mmoja kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambaye hakutaka jina lake kuwekwa wazi, alisema tayari mazungumzo yameshaanza baina yake na wakala huyo kwa ajili ya kumsajili John.

Kiongozi huyo amesema kinachofanyika sasa hivi ni mazungumzo ili kujua faida ya pande hizi mbili kama watakuja kufikiana mwafaka basi anaweza akaelekea United.

Aidha, mbali na United, imeelezwa pia baadhi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara zimevutiwa naye na zimeshaanza mazungumzo ya kimyakimya kuhakikisha zinapata saini yake.

7 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Hii stori haijakaa Vizuri. Wakala anaongeaje na TFF wakati Mchezaji ni wa AZAM...

    ReplyDelete
    Replies
    1. sio mchezaji wa azam huyo....anamilikiwa na kituo fulani cha michezo kilichopo mwanza.

      Delete
  3. Umeishiwa ndugu yangu... sio ili mradi upost story nyingi angalia na story yenyeye... taarifa haina chanzo cha kuamini ni wazi ni ta uongo

    ReplyDelete
  4. we jamaa hufai, mchezaji wa azam huy

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic