PAUL MAKONDA AALIKWA NA GAMBO KUZISHUHUDIA ARUSHA UNITED NA SIMBA
Na George Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amemualika Paul Makonda kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa kirafiki kati ya Arusha United dhidi ya Simba SC.
Makonda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ameitikia wito huo ili kwenda kushuhudia mechi hiyo ya kirafiki ambayo inapigwa leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini humo.
Gambo ameamua kumualika Makonda ambaye ni mnazi mkubwa wa Simba na akikubali wito huo hivyo tutarajie kumuona jukwaani kama mgeni rasmi.
Simba inaenda kucheza mechi hiyo zikiwa zimesalia siku 3 pekee kuelekea mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa jijini Mwanza Agosti 18.
Simba na Mtibwa watacheza mechi hiyo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ambao hivi sasa unamaliziwa kufanyiwa ukarabati tayari kwa kipute hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment