HAJI MANARA ATOA AHADI NZITO SIMBA
Ofisa Habari wa Simba SC, Haji Manara, amesema ataachia ngazi ndani ya klabu hiyo endapo timu yake itapoteza mchezo dhidi ya Arusha United leo.
Manara ametoa kauli hiyo kuelekea mchezo wa leo wa kirafiki ambapo Simba itacheza na Arusha United kufuatia mwaliko maalum na Mkuu wa Mkoa huo, Mrisho Gambo.
Ofisa huyo amefunguka akiamini kuwa Simba haiwezi kufungwa na Arusha United huku akitamba kumuahidi kipigo Gambo katika kipute hicho.
"Kama Arusha United wakishinda leo mimi nitaachia rasmi ngazi ndani ya Simba, siamini kama wanaweza wakatufunga" alisema.
Aidha, uongozi wa Simba umesema utautumia mchezo huo kama sehemu ya kuiandaa na mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Sugar.
Simba watakapiga na Mtibwa jijini Mwanza Agosti 18 ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba ukiwa unaahsiria kufunguliwa rasmi kwa pazia la Ligi Kuu Agosti 22 mwaka huu.
Uturuki na usajili wa mbwembwe na gharama kubwa huku mnaixhi kWa wcwc
ReplyDeleteAcha umama wewe wapi kumeonyesha wasi wasi????we unaona mtu anatoa kauli za kibabe kuonyesha anajiamini na chama uturuki alafu unasema tunaishi kwa wasi wasi...hujaona hapo jamaa kasema "Akifungwa kazi basi" ila siyo issue mashabiki wa yanga wengi ni brainless.
DeleteSawa
ReplyDelete