August 21, 2018


Ikiwa imesalia siku moja pekee kuelekea kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18, baadhi ya mashabiki wa Yanga wamewatambia Simba.

Jeuri hiyo wameipata kutokana na matokeo ya mchezo wa juzi kati yao na USM Alger kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Mashabiki hao wameeleza kuwa walikuwa wakiitwa vibonde lakini kwa namna kikosi chao kilivyowahenyesha Waarabu wamegeuza kibao na kuamini sasa kazi itakuwa ngumu kwa Simba kuutetea ubingwa.

Mbali na matokeo ya juzi, kitendo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji kuwasili Uwanjani kuwashuhudia vijana wake wakiwanyoa USM Alger, kimewapa nguvu mpya na hii ni kutokana na ugumu wa kipindi ambacho walikuwa wakipitia.

Manji aliwasili Uwanja wa Taifa kuitazama Yanga ikikipiga na Waarabu hao na uwepo wake ukawa na neema kwa kufurahia ushindi huo.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic