SINGIDA UNITED WAIAHIDI MAUMIVU SIMBA 2018/19
Uongozi wa klabu ya Singida United umetamba kufanya vema katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kutokana na usajili ambao imeufanya pamoja na namna wanavyojifua.
Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hemed Morocco, amesema kuwa aina ya wachezaji ambao timu imewasajili inawapa nguvu za kuchuana na vigogo ambao wamekuwa wakimaliza kwenye nafasi za juu msimu ujao.
Morocco ameeleza kwa namna ambavyo wamesajili kuna uwezekano mkubwa wakazipa changamoto Simba, Azam na Yanga kuwania nafasi za juu na ikiwezekana kuutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Aidha, Morocco amesema aina ya mazoezi ambayo anawanoa vijana wake, ana imani kubwa ya kufanya vizuri kwani wamekuwa wakifanya kila siku ili kuhakikisha makali yanakuwepo ligi itakapoanza.
Mbali na kujinoa kwa nguvu, Singida United wamekuwa wakicheza mechi kadhaa za kirafiki hapa nchini ambazo wanaamini zitawapa nguvu na morali ya kuendelea kujituma zaidi kupigania ubingwa msimu utakaoanza Agosti 22.








Hamna lolote ninyi walima alizeti
ReplyDeleteKazi ya Singida ni kuisaidia Yanga. Hawana haja ya kuishinda.
Delete