TAKWIMU ZA MAKAMBO KWA WAARABU YANGA NI HATARI TUPU
Alichokifanya straika, Heritier Makambo, Yanga iliposhinda mabao 2-1 dhidi ya USM Algiers kwenye Uwanja wa Taifa kinaonyesha kwamba jamaa ni jembe.
Takwimu za kile alichofanya Makambo dakika 90 zinaonyesha kuwa ni mchezaji hatari kama ataendelea kuonyesha juhudi akiwa na vijana hao wa Jangwani ambao sasa wana mzuka wa kurejea kwa Yusuf Manji.
Makambo ndiye alikuwa gumzo kwa mashabiki wa timu zote za Simba na Yanga ambao walihudhuriwa kwenye mchezo huo wa kimataifa ambao Yanga ilikuwa inakamilisha ratiba tu.
Kabla ya mchezo huo, Makambo alikuwa amefunga mabao matatu kwenye michezo mitatu ya kirafiki lakini aliendelea kuonyesha umahiri wake kwenye mechi hiyo baada ya kufunga bao moja kati ya mawili ya timu yake.
Katika dakika hizo tisini za Jumapili, Makambo aligusa mpira mara 24, huku akipiga pasi 18 zilizofika, alichezewa madhambi mara saba akiwa ndiye mchezaji aliyechezewa madhambi mara nyingi kwenye mechi hiyo iliyokuwa na mashabiki wachache.
Mbali na hilo, staa huyo ambaye kocha Mwinyi Zahera wa Yanga anasisitiza ni kifaa, alifunika tena kwenye kupiga mashuti ambapo alipiga jumla ya mashuti manne kwenye dakika zote alizocheza.
Mashabiki wa jukwaa la Simba wakati wa kutoka uwanjani walikuwa wakimzungumzia na kila mmoja alisifu kuhusu uwezo wake uwanjani ambapo aliibuka staa kwenye mechi hiyo.
Kacheza dk.90 kagusa Mpira mara 24 halafu unasema ana takwimu za kutisha.
ReplyDeletekagele ndo mwenye takwamu za kutisha kagusa mpira ma 6 tu Jana
ReplyDeletekagele ndo mwenye takwamu za kutisha kagusa mpira ma 6 tu Jana
ReplyDelete