Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa Ofisa Habari wake, Dismas Ten, umesema kuwa soka la Tanzania limekuwa likitawaliwa na wao siku zote.
Ten ameeleza hayo kutokana na klabu hiyo kutwaa taji la Ligi Kuu Bara mara 27 huku ikizizidi zote zote ambazo zinashiriki ligi hiyo.
Ofisa huyo ametamba akisema soka la Tanzania lipo chini yao huku akiwapiga dongo la kiaina Simba kuwa wanafanya baadhi ya mambo kwa kuwaiga.
Kiongozi huyo ambaye aliwahi kuwa Msemaji wa klabu ya Mbeya City ya Mbeya, amefunguka na kueleza kuwa kuna timu iliamua kuwaiga wao kwa kwenda Uturuki wakidhania kuwa wataweza kuchukua ubingwa wa ligi mara tatu mfululizo.
Hatua hiyo imekuja kufuatia Simba kusafiri hivi karibuni nchini huko na kuweka kambi ya wiki mbili kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi, kitu ambacho kimemuibua na kusema hawataweza kufanikiwa.
Aidha, Ten amewaomba mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa Jumapili ya wiki hii kukishuhudia kikosi chao kikicheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.
Yanga itakipiga na Waarabu hao majira ya saa 1 jioni ambapo mechi hiyo itakuwa LIVE kupitia Azam TV.








Hahaaa. Eti yanga inawacheka Simba wakati wao wenyewe hawajijui. Ama kweli ulimi hauna mfupi na huku wakitegemea bakuli badala ya Manji alieingia mitini, eti hawatambui kujiuzulu kwake. Poleni sana watani. Nawaomba wana Simba kesho wasiizomee Yanga ijapokuwa leo wao wanajikusanya kuizomea Simba dhudi ya Mtivwa kama walivoranfaza wenyewe
ReplyDelete