August 23, 2018




Yanga wameanza ligi kwa kutoa kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Pamoja na kwamba walionekana hawako vizuri, Yanga wameonyesha soka safi na kufanikiwa kushinda kwa mabao hayo, shujaa wakiwa Kelvin Yondani na Herietie Makambo raia wa DR Congo.

Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 31, Makambo akiunganisha vizuri kabisa.

Wakati ikionekana kama Mtibwa Sugar wangeweza kusawazisha, shambulizi la kushitukiza, dakika ya 39, Mrisho Ngassa aliangushwa ndani ya eneo la hatari na mwamuzi akaamuru mkwaju wa penalti upikwe.

Dakika ya 40, Yondania akaumwamisha mpira wavuni kwa ufundi maridadi akimuacha kipa Tinocco akianguka "halijojo".

Bao pekee la Mtibwa Sugar lilifungwa na Haruna Chanongo na Yanga wakashambulia zaidi mwishoni huku Tinocco akifanya kazi ya ziada kuokoa mkwaju matata wa Ibrahim Ajibu.


11 COMMENTS:

  1. Yanga nguvu ya soda na wamshukuru Mungu kwa kuponyoka kutoka kinywa cha mamba. Kipindi chapili chote kama tambara lililorowa maji, hawajiwezi, wakati Mtibwa ndio wakicheza ugenini, jee ungechezwa Manungu. Walikuwa taabani mikono kiunoni wanaomba duwa umalizike mpira kumnusuru Zuhera na aibu kuu. Ushindi walioupata sio wa heshima bali ni bahati tu. Ama Mtibwa walionesha kiwangu cha juu. Wachezaji wa yanga bila shaka watalala mapema kwa machofu.

    ReplyDelete
  2. Muandishi maneno tako kuhu kuwa yanga wakishambulia kwa nguvu kopindi chapili ni kinyuume kwani ni yanga walookuwa wakishambuliwa au kuonwa kutokana na hali ya uchofu uliopindukia mpaka

    ReplyDelete
  3. Hata simba walipata tabu kuwafunga mtibwa kule Arusha na mkafurahia kale kagoli kamoja vipi yanga iwe bahati wakatia wameingiza kambani goli mbili?

    ReplyDelete
  4. Simba angalieni team yenu ya 3bln,inashinda goli 5 kama jana

    ReplyDelete
  5. Wamewaotea tu na waamuzi wamewapendelea..VAR ingekuwepo ile penalty isingepigwa.Pili tangu lini mtu akaotea kwa mpira aliowapokonywa walinzi wa yanga. Mtibwa waliwazidi yanga kila kitu tangu ball possesion na shoot on target

    ReplyDelete
  6. Timu ya bilioni tatu imenona nanyi itazameni hali ya timu yenu ya Morogoro kipindi cha pili ni aibu alikuwa wapi Makambo wenu na mnyama wa Uturuki anakungojeeni

    ReplyDelete
  7. Wachezaji wengi wa Simba wanamzidi umri mdhamini wao (Mo). Nadhani Mo angewaona kabla hawajasajiliwa asingekubali kutoa fedha.

    ReplyDelete
  8. Goli la makambo alilogunga kwa kichwa mwamuzi wa pembeni akakataa ilikuwa co offside bali refa kachemsha. Yanga oyeeee

    ReplyDelete
  9. Yanga wamekataliwa goli zuri lisilo na dosari, tujiulize kwa nini?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic