September 4, 2018




Straika Mzimbabwe wa Azam FC, Donald Ngoma, amesema kwa sasa anajipanga kuweza kuisaidia timu yake katika mechi za Ligi Kuu Bara, ikiwemo kuhakikisha anafunga mabao ya kutosha msimu huu licha ya kuwa bado majeruhi.


Ngoma, raia wa Zimbabwe, amejiunga na Azam kwa mkataba wa mwaka mmoja akiwa anasumbuliwa na majeraha ya goti akitokea Yanga, kwa mkataba wa mwaka mmoja lakini bado hajafanikiwa kucheza mchezo wowote kwenye timu hiyo, kutokana na kuendelea na programu ya mazoezi mepesi kabla ya kuungana na wenzake. 


Ngoma alisema kuwa kwa sasa anachokiangalia ni jinsi ya kuweza kuisaidia timu yake kupata matokeo ya ushindi, kwa kuwa malengo yao ni kutwaa bingwa wa msimu huu katika Ligi Kuu Bara.

“Jambo kubwa kwangu katika kipindi hiki ni kuangalia nawezaje kuwa msaada kwenye timu yangu katika kila mechi kwa kuwa wakati wowote mwalimu anaweza kusema nirudi uwanjani kutokana na maelezo ya daktari licha ya mimi kuona nipo sawa.

“Unajua kitu kikubwa ambacho kipo mbele yetu ni suala la ubingwa, ndiyo ndoto ya kila mchezaji na hauwezi kupatikana  kama wachezaji tutashindwa kufunga mabao ya kutosha katika mechi zetu, ndiyo maana  najipanga vizuri ili tufikie malengo yetu msimu huu,” alisema Ngoma.    

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic