September 5, 2018


Baada ya taarifa kusambaa kwa kasi jana zikieleza kiungo mpya wa Yanga aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar, Mohammed Issa Banka, kufungiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) sababu za usajili wake zimewekwa wazi.

Banka alifungiwa na CAF wakati akiwa na timu ya Zanzibar kwenye mashindano ya CECAFA Challenge CUP nchini Kenya yaliyofanyika Novemba mwaka jana kutokana na kufeli vipimo vya afya.

Baada ya usajili huo kuleta gumzo huku wadau wengi na mashabiki wa Yanga wakishanaa ilikuwaje Yanga ikamsajili aliyefungiwa, siri imefichuka kilicho nyuma ya pazia juu ya usajili wake.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zinasema mabosi wa klabu hiyo wanajua fika kuwa Banka alikuwa tayari ameshafungiwa lakini waliamua kumsajili kwa faida ya baadaye.

Yanga kupitia Kamati ya Usajili ilifikia mwafaka na mchezaji huyo ambaye hivi sasa yupo Zanzibar akiendelea kujifua mchangani, waliamua kumsajili ili kumuandaa kwa ajili ya kuja kuitumikia timu hiyo siku za usoni.

Kutokuonekana kwa Banka tangu asajiliwe kulianza kuleta gumzo na maswali kwa wengi wakiuliza imekuwaje mpaka leo haonekani Uwanjani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic