September 29, 2018


Na George Mganga

Baada ya kushindwa kujumishwa katika kikosi cha Taifa Stars kilichoitwa na Kocha Emmanuel Amunike, imeelezwa kuwa beki wa Simba, Erasto Nyoni, amekubaliana kiroho safi na maamuzi ya kocha huyo.

Nyoni hajawa katika orodha ya wachezaji 30 waliotwa siku juzi na Amunike kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2019 dhidi ya Cape Verde utakaofanyika Oktoba 12 nchini kwao.

Nyoni ameeleza kuwa hawezi kupinga na hana tatizo na maamuzi ya Amunike kutokana na uteuzi wa kikosi chake bali atazidi kupambana kwa ajili ya kuisaka nafasi hiyo kwa hapo baadaye.

Mchezaji huyo kiraka anaamini bado umri wake unaruhusu kuendelea kuichezea Stars hivyo ataendelea kupambana ndani ya klabu yake mpaka atakapomshawishi Amunike aweze kumuita tena kwa mara nyingine.

Stars itaingia kambini hivi karibuni tayari kuanza maandalizi ya mechi dhidi ya Cape Verde tayari kusaka tikti ya kufuzu kucheza AFCON mwaka ujao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic