September 4, 2018


Wakati kkosi cha Yanga kikiendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mwinyi Zahera, amesema anawapa tizi la maana wachezaji wake kuhakikisha wanapata stamina.

Zahera ameeleza kuwa kikosi cha Yanga kina wachezaji wengi walio na ufundi pamoja na ubunifu ila kuna masuala kadhaa yanakosekana ambayo anayafanyia marekebisho kwa sasa.

Kocha huyo kutoka Congo, amesema lengo la yeye kuwapata tizi hilo wachezaji wake ni kuhakikisha kila mechi kwao inakuwa fainali ili kuutwaa ubingwa wa ligi.

Zahera ameeleza kuwa mechi zote za ligi kwake ni muhimu na anaziheshimu akisema si Simba pekee kwani ligi haina timu moja.

Ikumbukwe Zahera alisema Yanga inahitaji alama 30 pekee ikiwemo za Simba ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa ligi ambao ulichukuliwa na watani zao wa jadi msimu uliopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic