September 2, 2018


Wakati ligi ikiwa na siku kadhaa tangu kuanza, beki wa timu ya Yanga, Andrew Vincent, amesema kuwa safu ya ushambuliaji Simba ni moto wa kuotea mbali, imeelzwa.

Dante amesema hayo ikiwa ni takribani siku mbili kikosi cha Yanga kitue nchini kikitokea Rwanda ambako kilienda kushiriki mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Beki huyo anaamini safu hiyo ina makali kutokana na ujio wa straika hatari aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia FC, Meddie Kagere pamoja na uwepo wa Emmanuel Okwi na John Bocco.

Dante amesema licha ya Simba kuwa na makali mbele, watapambana kwa namna yoyote wanavyoweza ili waweze kuutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Katika msimu wa 2017/18 Simba waliwapoka Yanga waliotoka kuubeba mara tatu mfululizo na sasa Dante amesema watachuana kufa kupona ili waweze kuurejesha jangwani.

3 COMMENTS:

  1. Yanga wamezoea kuchonga.Hata walipoondoka kwenda Rwanda basi waliwafunga warwanda kabla hata hawajapanda ndege kuelekea huko. Timu amahayo itampa ushindani Simba katika ubingwa wa ligi ni Azam Fc peke yake wengine wote ni washindikizaji tu

    ReplyDelete
  2. Huyo jamaa awache kuropokwa kwakutaka kujipendekeza yanga. Ni juzi tu mme adhiriwa huko Ruwanda kwa kichapo baada ya porojo lenu kama hilo na huku eti mkisingizia mvuwa, mvuwa hiyo ilikunyesheeni nyie tu na Waruanda wakichezea ardhi isiyo na maji?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic