September 20, 2018


Unaambiwa jina la straika hatari wa klabu ya Simba, Meddie Kagere limezidi kutajwa na mashabiki wa Liverpool ya England kutokana na mshambuliaji wake Roberto Firmino kutumia staili ya ushangiliaji sawa na Kagere.

Liverpool ilishuka dimbani juzi kwenye Uwanja wa Anfield ikiwakaribisha PSG ya Ufaransa ambapo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Wakati matokeo yakiwa sare ya 2-2, Firmino aliingia mnamo dakika za mwisho za kipindi cha pili na kufanikiwa kupachika bao na kushangilia kwa kuziba jicho lake moja.

Staili ya ushangiliaji huo imewaibua mashabiki wa Simba ambao pia wanaishabikia Liverpool kutokana na ushangiliaji huo ambao unatumiwa na Kagere.

Ushangiliaji huo alioufanya Firmino uliwaamsha wanasimba na wapo baadhi walioanza kueleza kuwa amemuiga Kagere.

Wakati wakitamba hayo, kikosi cha Simba leo Alhamis kinashuka dimbani kucheza na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, mechi ikianza majira ya saa 10 jioni.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic