September 28, 2018


Baada ya Simba kubaki jijini Dar na kuweka kambi katika Hoteli ya Sea Scape iliyopo Mbezi Beach, jana Jumatano kikosi hicho kilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko.

Katika mazoezi hayo, uongozi wa Simba uliwawekea ulinzi mkali nyota wake hao kuelekea mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Yanga utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Katika mazoezi hayo ya jana, licha ya mashabiki kuwepo hapo uwanjani lakini kulikuwa na makomandoo kadhaa ambao walikuwa wanazungu kazunguka wakati mazoezi yakiendelea.

Hata hivyo, katika mazoezi hayo, wachezaji wa Simba walionekana kufanyishwa mazoezi ya nguvu na makocha wa kikosi hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic